NA MWANDISHI MAALUMU,UGANDA
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba na Waziri wa Uhamiaji na Bima ya Taifa wa Bahamas, Alfred Sears wamesisitiza umuhimu wa nchi zao kuchukua hatua za haraka kuanzisha ushirikiano rasmi kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili.
Msisitizo huo umefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) unaoendelea jijini Kampala, Uganda kuanzia Januari 15 hadi 20 , 2024.
Maeneo ya ushirikiano yatakayopewa kipaumbele ni pamoja na kukuza sekta ya utalii, biashara na Uwekezaji, michezo na utamaduni .