NA MUNIR SHEMWETA,KILIMANJARO
NAIBU Waziŕi wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda ameshiriki katika mazishi ya mtumishi wa Wizara ya Ardhi Makao Makuu Joyce Shayo.
Mazishi hayo yaliyohudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Lucy Kabyemera yamefanyika katika eneo la Uru mkoani Kilimanjaro Januari 3,2024.
Marehemu Joyce Shayo alifariki 3l Desemba 30, 2023 katika Hospitali ya Amana jijini Dar Es Salaam akisumbuliwa na Shinikizo la Damu.
Marehemu atakumbukwa zaidi kwa kuwa sehemu ya timu ya wataalamu waliokuwa wakifanya kazi ya Utatuzi wa Migogoro ya Matumizi ya Ardhi katika vijiji 975. Marehemu ameacha watoto watatu.