NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC) limekiri kutoridhishwa na hali ya eneo la mapokezi ya abiria wanaosfiri kati ya Dar es salaam kwenda Zanzibar na kutoka Zanzibar kuingia Dsr es salaam
Aidha kutokana na kutokuridhishwa na hali eneo hilo imeazimia kulifanyia marekebisho kwa kushirikiana na MAmlaka ya Usimamizi wa Bandari.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo Nelson Mlali alipozungumza na Wahariri wa Vyombo vya habari ikiwa ni mwendelezo wa Taasisi za serikali kuufahamisha umma juu ya mafanikio na changamoto ya Taasisi hiyo na Serikali ya swamu ya sita kwa ujumla.
Mlali alisema ni kweli sio nzuri na hairidhishi lakini jitihada za haraka zinafanyika kuinusuru hali hiyo ili kuondoa kero hiyo kwa manufaa ya abiria na watumiaji wa bandari ya Dar esalaam.
Akizungumzia mafanikio Mlali alisema tangu Tasac ianzishwe mwaka 2018 limeendelea kuwa na mafanikio makubwa kimapato hadi kufikia Sh.Bilioni 43.5 kwa mwaka 2021/22 kutoka Bil.9.1 ya mwaka 2018/19
“Mafanikio haya yametokana na usikivu wa Serikali katika kupokea ushsuru wa kitaalamu na kutoa maelekezo sahihi kwa wizara ya Uchukuzi” alibanisha Mlali
Alisema Tasac imeongeza idadi ya usajili wa Mabaharia 1038 mwaka 2021/22 kutoka 796 kwa mwaka 2018/19.
Mbali ya hayo pia Tasac imeongeza idadi ya usajili wa leseni kutoka 145 kwa mwaka 2018/19 hadi 240 kwa mwaka 2021/22
“Shirika limeongeza idadi ya vyeti vinavyotolewa na kwa mabaharia waliokidhi vigezo kufikia 17689 mwaka 2021/22 kutoka 5, 699 mwaka 2018/19.Lakini pia leseni za vyombo vidogo zimeongezeka hadi kufikia 6366 kwa mwaka 2022 kutoka 2006 kwa mwaka 2018” alihitimisha Mlali