NA DANSON KAIJAGE,BARIADI
LICHA ya Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa kufanya kazi za Serikali kwa kiwango cha juu hususani katika usimamizi wa miradi ya ujenzi wa barabara lakini bado amekuwa hakijikita hata kwenye shughuli za kijamii na kiibada.
Hali hiyo imejidhihirisha leo Oktoba 8 mwaka huu baada ya Bashungwa kushiriki katika Misa Takatifu kwa ajili ya kuongoza harambee ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Luka Jimbo la Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri Bashungwa akitoa taarifa baada ya harambee hiyo amesema kiasi kilichopatikana ni Milioni 28.8 ambapo ni pesa taslimu na ahadi.
Aidha, Waziri Bashungwa ametoa wito kwa waamini walioshiriki Misa hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa nia ya kuunga mkono Seriikali inayoongozwa na Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan.
Kanisani hapo Bashungwa pia amehamasisha zaidi suala la kulinda amani ya nchi pamoja na kujenga misingi ya mshikamano na kuwafanya watanzania kuwa wamoja.
Waziri huyo wa Serikali ya Rais Samia amewataka waamini kuhakikisha wanakuwa kielelezo kwa jamii na kunenea mema Tanzania huku akitaka kuhakikisha wanashirikiana na serikali katika shughuli za maendeleo.
Waziri Bashungwa ameshiriki Misa hiyo mwendelezo wa ziara ya kikazi katika katika Mikoa ya Mbeya, Iringa, Singida, Simiyu na ataendelea katika Mkoa Mara, Mwanza na Kagera.