NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imetangaza kushiriki maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika Uwanja wa Maonyesho wa Biashara wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 28 hadi Juni 13, 2023.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 30, 2023 na Taasisi hiyo, Katika maonesho hayo itafanya upimaji na kutoa ushauri wa kiafya kuhusiana na magonjwa ya moyo, kuelezea kwa kina huduma zinazotolewa na Taasisi na kutoa matibabu ya hapohapo kwa wagonjwa wanaokutwa na matatizo ya moyo yanayohitaji kupewa rufaa.
Madaktari mabingwa wa magonjwa ya moyo Tulizo Shem, Tatizo Waane, Delilah Kimambo, Honaratha Maucky, Baraka Ndelwa na Pedro Pallangyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dk Peter Kisenge watakuwepo katika banda lao kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi.
Aidha JKCI imesema inawakaribisha wananchi wote kutembelea Banda letu lililopo ndani ya banda la Jakaya Kikwete ili kupata huduma mbalimbali zinazohusiana na afya ya moyo
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ipo kwaajili ya kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora na kuwa na elimu inayohusiana na magonjwa ya moyo.