NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
JESHI la Polisi nchini Tanzania linawashikilia watu 13 kwenye mahabusu ya ofisi za Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakiwatuhumu kwa kuandamana.
Akizungumza na DEMOKRASIA, wakili wa waliokamatwa, Dickson Matata amesema wateja wake walikamatwa leo Jumatatu, Juni 19 katikati ya mji wa Dar es Salaam wakituhumiwa kuandamana.
Matata amesema Polisi wanaendelea kuchukua maelezo ya watu hao na wamesema watawaachia kesho Jumanne.
DEMOKRASIA liliwasiliana wanaharakati wa Sauti ya Watanzania ambao walishiriki kuandaa maandamano hayo na kupata baadhi ya majina ya waliokamatwa kuwa ni Deusdedith Soka, Remina Peter, Fatma Thabit, Joel Msuya, Mchewa, Alphonce, Kaswahili, Haji na Nita.
Maandamano hayo yaliyoasisiwa na Mwanaharakati Deusdedith Soka na kuungwa mkono na wanaharakati wengine inaelezwa yana lengo la kufikisha ujumbe kwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan asikubali Tanzania kuingia mkataba na Serikali ya Dubai ya kuendesha bandari.
PICHA: Mwanzo TV
SOMA ZAIDI: