NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
BENKI ya CRDB imeianza safari ya wiki mbili ya kuwapika wabunifu 196 waliochaguliwa kwenye programu yake ya Imbeju inayolenga kutoa mtaji wezeshi kwa vijana na wanawake.
Washiriki hao ni kati ya wabunifu 709 waliotuma maombi yao kuanzia Machi 12 programu hiyo ilipozinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kukidhi vigezo vya awali vilivyowekwa.
Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amewapongeza washiriki waliofanikiwa kufika hatua hii akiwasisitiza kuwa ubunifu wao wa kipekee, shauku yao isiyoyumba, na jitihada zao katika ujasiriamali zimewaweka mbele ya kundi kubwa la washiriki waliowasilisha maombi yao hivyo kuwa sehemu ya fursa hii.
“Tunapoianza kambi hii ya mafunzo, ni wakati muhimu katika safari yenu ya ujasiriamali kwani mtapata fursa ya kuboresha bidhaa na huduma zenu, mikakati na kupata ujuzi muhimu unaohitajika ili kuwawezesha kufanikiwa katika hatua hii ya mwanzo katika uendeshaji wa biashara.
Niwasihi kujifunza kwa umakini mkubwa ili kutumia mafunzo na uzoefu mtakaoupata kuboresha biashara zenu. Kumbukeni kuwa maarifa ni nguvu na kwa kujijengea ufahamu na ujuzi sahihi, mtakuwa tayari kukabiliana na changamoto na kuchukua fursa nyingi zilizopo mbele yenu. Na hapo ndipo mafanikio ya programu hii yatakapoonekana,” amesema Nsekela.
Mkurugenzi huyo pia alisisitiza dhamira isiyoyumba ya Benki ya CRDB kusaidia kukuza biashara changa nchini kupitia mitaji wezeshi hasa zile zinazomilikiwa na vijana na wanawake, makundi muhimu yasiyopewa kipaumbele kwenye fursa za uchumi.
Nsekela amesisitiza kuwa Benki ya CRDB inaelewa kuwa upatikanaji wa fedha ni jambo muhimu katika kubadilisha mawazo bunifu kuwa biashara endelevu hivyo programu ya IMBEJU inalenga kuchochea mafanikio ya wabunifu na waanzilishi wa biashara na kuhakikisha fedha haiwi kikwazo cha safari yao ya ujasiriamali.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa amesema wanatambua kuwa mtaji si kikwazo pekee cha vijana wenye mawazo bunifu kuyageuza kuwa biashara inayotatua changamoto za jamii kwani takwimu zinaonesha biashara nyingi changa zimekufa si kwa sababu ya mtaji bali kutokana na kukosa maarifa sahihi ya usimamizi na uendeshaji wa biashara.
“Leo tupo hapa kutekeleza kile tulichoahidi kwa maana ya kutoa mafunzo yanayolenga kuwaongezea uwezo vijana walioomba mtaji wezeshi wa Imbeju ili ikifika hatua ya kuwawezesha kwa mtaji, wawe tayari kutumia mtaji huo kwa ufanisi na kuleta matunda yaliyokusudiwa.
Katika hatua nyingine , Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk Amos Nungu alisema wanaamini mtaji ni fedha tu bila kufahamu kuwa hata wazo pekee ni mtaji ambalo mwenye nalo akishikwa mkono anaweza kulifanya biashara