DAR ES SALAAM, TANZANIA
Kampuni za simu za mkononi Infinix inafanya jitahada nyingi katika kupanua Teknolojia ya Mawasiliano nchini, na hii ni baada uzinduzi wa toleo jipya la simu ‘series’ ya NOTE 30.
Infinix kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali, juzi ilizindua rasmi promosheni ya ‘GusanishaIjae’ huku mpango mkakati ukiwa ni kuwanufaisha watanzania wengi kupitia teknolojia ya mawasiliano.
Promosheni ya Gusanisha ijae iliongonzwa na Mtangazaji maarufu wa Clouds Media, Meena Ally pamoja na Dancer wa Muziki wa Kizazi Kipya, Chino ambapo Meena Ally alikabidhi kitita cha Shillingi Milioni 1 (1,000,000/-) kwa mteja ambaye alinunua Infinix NOTE 30 Pro na zawadi nyingine nyingi zilienda kwa wateja wengine wa siku hiyo zikiwemo Microwave, Blenda, Airflier n.k.
Chino pamoja na kundi lake walitoa burudani ya kutosha kuhakikisha watu wanafika kwa wingi na kwa pamoja kuhakikisha lengo linafikiwa la kutengeneza mazingira rafiki kwa wateja wa simu janja.
Kwa mujibu wa Meena Ally alisema fursa bado zipo nyingi sana hasa kwa mwezi huu ambao simu pekee inayotingisha mtaani kuwa na teknolojia bora ya kuchaji haraka (fast charge) ikiwa na Watts 68 na Wireless chaji ya Watt 15 imeziduliwa. Pia amewataka watanzania wengi kujitokeza kwa wingi sehemu husika wakisikia tu Infinix wana jambo lao.
Ikumbukwe kupitia Infinix NOTE 30 imetolewa ‘offer’ kwa Mwezi huu Juni kukopa simu hii inayopatikana kwa Tsh.650,000 za Kitanzania pasipo Riba na kwa huduma hii tembelea maduka yao yote ya simu nchini au tembelea mitandao ya jamii kwa anuani ya @infinixmobiletz au piga 0745170222.