NEW YORK, MAREKANI
Trey Songz, mkali wa miondoko ya RnB raia wa Marekani anatarajia kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumnyanyasa mwanamke kijinsia.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Trey anatuhumiwa kushika titi la mwanamke na kulichomoa nje ya sidiria kwenye halaiki wakati wakiwa kwenye ukumbi mmoja wa starehe.
Msichana huyo anayeitwa Jane Doe akiwakilishwa na Wakili wake, tayari walishamtumia barua ya madai mwanamuziki huyo kwenye tukio hilo lililotokea mwaka 2013.
Barua hiyo ilieleza kuwa mwanamuziki huyo alifanya tukio la kuchomoa ziwa la Jane bila idhini yake na kufanya watu wote waone sehemu hiyo ya siri ya mwanamke huyo kwenye sherehe iliyoandaliwa na Trey Songz.
Wakili wa mwanamke huyo amesema mteja wake amedhalilishwa na kuathiriwa kisaikolojia tangu wakati huo mpaka leo tukio hilo limekuwa linamsumbua.
Kwenye barua hiyo Jane amedai fidia ya Dola za Marekani Milioni 10 (Tsh. Bilioni 22.3) la sivyo watapeleka shauri hilo mahakamani.