DAKAR, SENEGAL
HUDUMA ya Intaneti nchini Senegal imezimwa baada ya kutokea vurugu zilizosababisha vifo vya watu 16 na wengine zaidi ya 350 kujeruhiwa.
Serikali ya nchi hiyo imefikia uamuzi hayo baada ya watu kuandamana na kutokea vurugu kali nchini humo baada ya kiongozi Chama cha upinzani, Ousmane Sonko kuhukumiwa kwenda jela miaka miwili.
Sonko alikutwa na hatia ya kumnyanyasa mwanamke kingono kwenye nyumba chaa kufanyia massage lakini wakati wa kutolewa hukumu hiyo mwanasiasa huyo hakuwepo mahakamani.
Waziri wa haki wa nchi hiyo alisema wameshaweka taratibu za kumkamata muhukumiwa huyo na tayari Polisi wapo doria nyumbani kwake.
Wafuasi wake wakaanzisha maandamano wakipinga hukumu hiyo wakidai imetengenezwa ili kumfanya asigombee kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.