DENIS CHAMBI,KILINDI
ZAIDI ya wakazi 7000 wa kijiji cha Msamvu Kata ya Tunguli Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga wanakabiliwa na ukosefu wa kituo cha afya hali inayowalazimu kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 90 kufuata huduma hiyo.
Kutokana na changamoto hiyo vifo vya wajawazito katika kijiji cha Msamvu kata ya Tunguli wilayani Kilindi mkoani Tanga vimekuwa ni jambo la kawaida hivyo kuwalazimu kufuata huduma hiyo Gairo wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM )Mkoa wa Tanga Rajab Abdurahamani ameshangaa kuona kituo cha afya kinachojengwa kwenye eneo hilo kikiwa bado hakijakamilika licha ya serikali kutoa Sh. Milioni 400 toka mwaka 2021.
“Serikali imeleta fedha kwa muda mrefu tokea 2021 hadi leo haijamalizika huu ni ujanja ujanja tu ninaouona hapa mheshimiwa DC hawa watu kuwa mkali wasikuchezee mheshimiwa Rais amekuamini kwamba hii kazi unaiweza mheshimiwa Rais atafoka kwa kalamu wewe foka kwa mdomo ili mambo haya yaende kwasababu chama hiki kilikuja hapa kikaomba kura kwamba mkitupa ridhaa tutawaondolea changamoto kwenye huduma za afya leo serikali imeleta fedha lakini majengo hayakamiliki kwa wakati mwisho wa siku kinatukanwa chama cha mapinduzi sisi hatuwezikukubali ndugu zangu chama hichi kikatukanwa hatuwezi kukubali, “amesisitiza Mwenyekiti
Akitoa sababu za kuchelewa kwa kituo hicho mtendaji wa kata hiyo Omari Mtoi amesema kuwa kuchelewa kwa ujenzi wa kituo hicho kunatokana na umbali mrefu ambao wananchi walikuwa wakitumia kuchota maji kwajili ya ujenzi lakini pia ugumu wa eneo hilo kufikika wakati wa kupeleka vifaa vya ujenzi.
Katika hatua nyingine CCM Mkoa wa Tanga wameanza kuwashughulikia wenyeviti wa mitaa ambao wanahusishwa na migogoro ya ardhi hususani katika kipindi hiki ambacho chama hicho kinaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa huku wakitoa msimamo wa chama hicho wa kwamba
Pia chama hicho kimetoa msimamo wa kuwataka viongozi wasio waadilifu wawapishe ndani ya chama hicho kwani chama kinataka viongozi waadilifu wanaofanana na kasi ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Katika ziara yake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Abrahaman na katibu wa chama hicho Suleiman Mzee wamewataka wanachama wa chama hicho kuwapuuza viongozi wenye nia ya kurudi madarakani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wakati ndio walikuwa chanzo kikubwa cha migogoro ya ardhi.
“Viongozi wa kijiji na serikali yake ya kijiji mnatuletea matatizo ya migogoro ya ardhi mwishowa siku DC analaumiwa, mkurugenzi analaumiwa kwa kuuza ardhi ovyo halafu mnatuambia mwakani tuwarudishe tena viongozi hawa kiukweli hatuwarudishi viongozi hawa hata kama mnawapendaje kuna watu wamepewa hekari 100 heka 200 hadi heka 1000 hiyo ni kinyume cha taratibu kwasabab hata kama mkutano wa kijiji umeamua haiwezekani kutoa eneo zaidi ya heka 50 ambazo zinatakiwa kuamuliwa na Halmashauri husika, “
“Huku watu wanatoa ardhi kiholela mheshimiwa mkuu wa wilaya fuatilia na kamati yako ya ulinzi na usalama wale wote waliopewa ardhi kinyume na utaratibu ardji hiyo irudi serikalini ili yaondoe migogoro hiyo ya ardhi haiwezekani tukafumbiana macho ndugu zangu chama hichi ni kwajili ys kuwatetea wanyonge chama hichi ni chama kinachopigania wale wote ambao wameonekana wapo chini wapo duni ndio kazi ya chama hiki hatuwezi kukubali kila aliyehusika kunyakua, ardhi ya serikali kinyume na utaratibu awajibike, “amesisitiza Mwenyekiti huyo
Kwa upande wake katibu wa chama hicho Suleiman Mzee amesema wapo watu ambao walishirikiana na watu waovu wakasimamia kuuza ardhi bila kushirikisha wananchi kama wapo mkurugenzi wa uchaguzi anassma kwamba wawapishe ndani ya chama hicho kwakuwa chama kinataka viomgozi waadilifu wanaofanana na kasi ya Dk Rais Samia Suluhu Hassan.
“Wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji mpo hapa hebu nyoosheni vidole muda wa kujirekebisha upo, usipojirekebisha sasa kama ulisahahu jana imekula kwako chama hichi baada ya kuchaguliwa mlipewa miongozo mtakabidhiwa wananchi na mipaka mzingatie usalama wa wananchi wetu lakini muwashirikishe katika maendeleo yao wapo wenyeviti waliofanya vizuri na wapo wenyeviti ambao hata hilo jambo hawajafanya na kama hawajafanya muda unafika waswahili wanasema kutesa kwa zamu, “amesema Katibu Mzee
Moja ya changamoto wanayokutana nayo viongozi hawa ni pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara kuanzia mpaka wa Gairo wilayani Mvomero hadi katika katika Wilaya ya Kilindi.