NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) nchini, Manfredo Fanti katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika sekta mbalimbali hususan za Biashara na Uwekezaji, elimu, afya, utalii, nishati, mitindo, utamaduni, uchumi wa buluu, mifugo na uvuvi.