–
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KATIKA kuhakikisha mgomo wa wafanyabiashara wa kariakoo unapatiwa ufumbuzi leo Mei 15, 2023 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefika katika Soko hilo na kuzungumza na wafanyabiashara hao ili kutafuta suluhu.
Ziara hiyo ya Majaliwa imekuja saa chache baada ya Ofisi ya Waziri Mkuu kutoa taarifa ya uwepo wa mkutano baina yao Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, TRA na Mawaziri husika katika Ikulu ya Magogoni Mei 17 mwaka huu.
Waziri Majaliwa amesema kuwa amelazimika kuacha Bunge na kuja kwa dharura ili kuzungumza na wafanyabishara hao kwa lengo la kupata suluhu.
Katika mkutano huo Waziri Mkuu Majaliwa aliagiza kusitishwa kwa Kikosi kazi cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambacho kilifutwa mwaka jana lakini kiliendelea kufanya kazi kinyemela kwa madai ya kufanya kazi kwa kuwakandamiza wafanyabiashara
Mbali ya hilo Majaliwa aliagiza wafanyabiashara hao wasibughudhiwe kwa namna yeyote ile kwani amepokea malalamiko kutoka mikoa mbalimbali
Hata hivyo, wafanyabiashara hao hawakusitisha mgomo huo na kudai kutaka kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan.