NA MWANDISHI WETU, TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ameelekeza Vikao vyote kuhusu Mradi wa Bomba la Mafuta kuanzia sasa vifanyike Mkoani Tanga kwa lengo la kuhamasisiha wananchi zaidi kuhusu mradi huo.
Kindamba ameyasema hayo leo Mei 15, 2023 wakati wa kikao cha mrejesho wa utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta kilichofanyika mkoani Tanga.
“Ni muhimu vikao vyote vifanyike Tanga baadala ya kufanyika Dodoma au Dar es Salaam, mkivifanya hapa sisi watu wa Tanga tutanufaika moja kwa moja” amesisitiza Kindamba.
Aidha amewataka Waratibu wa Mradi wa Bomba la mafuta kwa kila wilaya kuhakikisha wanafanikiwa kusaidia makampuni na wananchi kuweza kufaidika na mradi huo.
“Kuanzia sasa bila kufumba macho muanzishe kanzidata ya makampuni na watu ambayo mumefanikiwa kuwasaidia katika Mradi huo Wakurugenzi na Makatibu Tawala wa Wilaya simamieni fursa hiyo kwa ajili ya wananchi wa Tanga” amesisitiza zaidi.
Amesema kutokana na utamaduni ya Mkoa wa Tanga lazima tuwashike mikoni kuwasaidia wananufaidika na mradi huu, kwani kilio kikubwa cha kwamba wana Tanga hawajafaidika na mradi wa bonba la Mafuta sitaki kuisikia katika kipindi changu.
Lengo la Serikali ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kuona Watanzania zaid wananufaidika na Mradi hivyo hii ni fursa ambayo lazima tuitumie.