NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amesema serikali inafuatilia tetesi za uwepo wa Uviko- 19 nchini.
Akitoa taarifa kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii amewaondoa hofu wananchi na kuwaomba kutulia wakati wanafuatilia suala hilo.
“Wizara ya Afya inachakata taarifa zilizokusanywa kutoka Hospitali/Vituo mbalimbali ndani ya wiki hii tutatoa taarifa kama kuna ongezeko la magonjwa ya mfumo wa hewa au lah!” amesema Ummy na kuongeza
“Kwa taarifa za wagonjwa waliopimwa virusi vya Uviko -19 wiki ya kuanzia Mei 6 hadi Mei 12, 2023, watu sita kati 6 ya 288 walithibitishwa kuwa na corona ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya Aprili 29 hadi Mei 05,2023, hakuna kifo chochote kilichothibitishwa kusababishwa na Uviko -19. “amesema
Amesema, wizara ya afya inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye Hospitali mbalimbali na kwamba watatoa taarifa kamili.
“Nawaomba wananchi muendelee kuzingatia kanuni za afya na usafi.”ameeleza