NA MWANDISHI WETU, TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Sipora Liana pamoja na watendaji wake kuendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuendelea kukusanya zaidi kutoka makusanyo ya shilingi bilioni 18 hadi kufikia bilioni 30 .
Kindamba ameyasema hayo katika Kikao cha watumishi na Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri ya hiyo kilichofanyika leo Mei 3, 2023.
“Tuna bilioni 18 lakini tunauwezo wa kukusanya bilioni hata 30 tuendelee kukaza mwendo vyanzo vyote vile ambavyo vimejifichaficha twendeni tukaving’amue” amesema Kindamba.
Wakati huo huo, RC Kindamba anewataka watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ana matarajio makubwa na Mkoa huo kwa kuwekeza katika miradi mikubwa ya maendeleo .
“Mheshimiwa Rais ana matarajio makubwa na mkoa wa Tanga na ndio maana amemimina fedha nyingi katika bandari yetu zaidi ya bilioni 429.1 katika maboresho yake hivyo tufanye kazi fursa zipo” amesisitiza Kindamba


