NA MWANDISHI MAALUM, TANGA
HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imefanikiwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kufanya mabadiliko ya kiutendaji kutoka kwenye mfumo wa zamani na kuhamia katika matumizi ya mfumo wa kisasa kwa kununua Vishikwambi 64 kwa ajili ya Madiwani, Wakuu wa Idara, Vitengo vya Halmashauri hiyo
Vishikwambi hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Tshs. Milioni 101 zime gharamiwa na Halmashauri ya Jiji hiyo.
Akikabidhi vitendia kazi hivyo Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Pili Mnyema amesema kuwa lengo la kuhamia katika Mfumo wa Digitali ni kuokoa gharama ambazo zimekuwa zikitumika kwa ajili ya uendeshaji wa vikao ndani ya Halmashauri.
“Kwa kuingia kidijitali sasa hamna umuhimu sana wa kuingia gharama ya kuchapisha karatasi, kwani matumizi ya Teknolojia ya Vishikwambi itamaliza tatizo hilo.
Aidha ameipongeza Halmashauri ya Tanga kijumla kwa kuingia kidijitali na kuwataka watumishi hao wa Halmashauri kuhakikisha wanavitunza vifaa kwa kuongeza tija na ufanisi kwenye shughuli za kikazi zao.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Jiji la Tanga Dk. Sipora Liana amesema kuwa vitendea kazi hivyo vitaboresha utawaka bora na kwamba itakuwa halmashauri ya pili kwa manunuzi na ugawaji wa vishikwambi nchini baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.