KILIFI, KENYA
IDADI ya miili ya waumini waliofariki dunia kwa kufunga imefikia 65 katika shughuli za ufukuaji wa makaburi zinazoendelea katika Kaunti ya Kilifi nchini Kenya.
Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti mchungaji huyo alikamatwa siku 10 zilizopita na Jeshi la Polisi katika Kaunti ya Malindi nchini humo baada ya kudaiwa kuwashawishi waumini wake wafunge hadi kufa ili waingia mbinguni na kuurithi ufalme wa Mungu.
Akizungumza Aprili 24, 2023 wakati wa shughuli hiyo, Inspekta Jenerali wa Polisi, Japhet Koome amesema baada ya kufika eneo la tukio na kushuhudia miili mingine 26 ikifukuliwa hivyo kufikia 65 waliokufa. Amesema watu 29 waliokolewa na kupelekwa hospitalini.
IG Koome na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mohammed Amin walifika kijijini hapo mchana kufuatia ufukuaji huo huku uchunguzi ukiendelea kuhusu njaa na kusababisha vifo hao.
Jeshi hilo limeingia wasiwasi huenda baadhi hawakufa kwa njaa kabla ya kuzikwa kwenye eneo hilo.
Tukio hilo lililoibua mjadala katika ukanda wa Afrika na dunia limeendelea kuibua maswali kuhusu uwajibikaji wa vyombo vya usalama vya ndani nchini humo hatua iliyoibua hisia na mjadala unaoshambulia Serikali katika mwenendo wa kushughulikia kesi hiyo.
Aprili 24, 2023 Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Ndani Profesa Kithure Kindiki amesema Serikali itaendelea kuheshimu uhuru wa dini lakini adhabu kali kwa mhusika lazima itatolewa.
“Mauaji hayo ni unyanyasaji zaidi wa haki ya binadamu ya uhuru wa kuabudu kikatiba, sheria za Kenya pamoja na sheria za kimataifa.
“Wakati Serikali inaendelea kuheshimu uhuru wa dini, dosari hii lazima itoe adhabu kali zaidi ya mhusika huyu (mchungaji) kwa kupoteza uhai wa watu wasiokuwa na hatia, lakini udhibiti mkali zaidi uonekane kwa kila kanisa, msikiti, hekalu au sinagogi,” amesema Profesa Kindiki