NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KATIKA kutambua umuhimu wa Usalama kwa vyombo vya Moto hapa nchini hususani madereva wa pikipiki maarufu kama Bodaboda, Meridianbet Tanzania imeanzisha kampeni inayoitwa Mtaa Kwa Mtaa Na Meridianbet yenye lengo maalum la kugawa viakisimwanga kwa madereva wa bodaboda wa maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jeshi la polisi la Usalama Barabarani.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo, Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Matina Nkurlu, aliyeambatana na timu ya masoko kutoka Meridianbet alisema wameamua kushirikiana na jeshi la Polisi la Usalama Barabarani kutoa elimu ya Usalama barabarani pamoja na kugawa reflectors kwa madereva bodaboda.
Sababu ya kufanya hayo kupunguza ajali nyingi sana hususanI nyakati za usiku na ndiyo maana wameamua kutoa reflectors kwa madereva wa bodaboda wote waliopo jijini Dar es Salam, maeneo yaliyofikiwa hadi sasa ni Kawe, Kinondoni, Sinza, Mwenge na Tangibovu huku lengo ni kuwafikia madereva bodaboda wote wa jiji lote la Dar es Salaam.
“Meridianbet tuna msemo wetu wa CHAGUA TUKUPE, huu ni maalum kwa wateja wetu wote kuwa tunawapatia kile wanachotaka, baada ya kusikia kilio cha madereva hawa wa Bodaboda tumeamua kuwapatia Reflectors hizi maalum ili kujikinga na majanga ya barabarani kama ajali lakini pia ni kuimarisha usafi na utanashati wao binafsi”alisisitiza Nkurlu