NORTH WALES, MAREKANI
KUNDI kubwa la Mbuzi wenye tabia ya kuzurura katikati ya mji kwa zaidi ya miaka 100 wameachiwa huru baada ya kushinda kesi ya uzururaji nchini Marekani
Baraza la Halmashauri ya Llandudno, North Wales iliamuru mbuzi hao kuwa huru licha ya tabia mbovu walizonazo wanyama hao za kula mimea na uzio wa nyumba za watu.
Kutokana na kusababisha maafa kwa jamii mara kadhaa wakazi wa Wales wamekuwa wakitaka kuwapiga risasi mbuzi hao ili watoweke kwenye makazi ya watu.
Mamlaka ya ya eneo hilo imeamua kuwa ni jukumu la wamiliki wa ardhi kulinda mali zao dhidi ya Mbuzi hao wazururaji badala ya kuzuiliwa.
Ripoti ya mwisho iliyotolewa na Baraza imewapa haki Mbuzi hao wa ‘Kashmir’ ikisema kwamba hawatawafungia wanyama hao ili wasizurure na badala yake wapo huru.