WAKAYAMA, JAPAN
WAZIRI Mkuu wa Japan, Fumio Kishida amenusurika kifo baada ya kurushiwa bomu leo Aprili 15, 2023 katika eneo la Wakayama nchini hapa.
Tukio hilo limetokea katika eneo la hadhara ambapo Waziri Mkuu huyo aliandaliwa kwaajili ya kutoa hotuba kwa vyombo vya habari.
Pamoja na shambulio hilo Waziri Mkuu Kishida amenusurika pasipo kupata majeraha yeyote.
Hata hivyo mwanamume mmoja aliwekwa kizuizi katika eneo hilo baada ya kuhisiwa kuhusika na tukio hilo.
Waziri Mkuu Kishida alipaswa kutoa hotuba kwa vyombo vya habari vya eneo hilo.
Shuhuda mmoja alisema waliona mtu akirusha kitu, na kufuatiwa na moshi, huku mwingine akisema walisikia kishindo kikubwa hata hivyo hakuna majeruhi walioripotiwa.
Shirika la utangazaji la umma la Japan, NHK, lilimnukuu Kishida akisema kulikuwa na “mlipuko mkubwa kwenye ukumbi huo. Polisi wanachunguza maelezo, lakini ningependa kuomba radhi kwa kuwatia wasiwasi watu wengi na kuwasababishia matatizo.”