KABIRDHAM, INDIA
NDUGU wawili wa familia moja wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa kwa kulipukiwa na bomu wakiwa kwenye sherehe ya harusi baada ya kupokea zawadi ya keki wilaya ya Kabirdham nchini India
Mmoja wa marehemu hao ni bwana harusi ambaye alikuwa ametoka kufunga ndoa hivi karibuni .
Polisi wanasema zawadi hiyo iliwekwa bomu ambalo lililipuka muda tu ilipowekwa katika umeme.
Wakati bwana harusii akifariki papo hapo, kaka yake alifariki kutokana na majeraha wakati wa matibabu.
Polisi walisema kuwa bomu hilo lilidaiwa kutumwa na aliyekuwa mpenzi wa bibi harusi ambaye alikuwa na hasira dhidi yake kwa kuolewa na mume mwingine.
Mshtakiwa, ambaye ametambuliwa kama Sarju Markam(33) kutoka jimbo jirani la Madhya Pradesh, alikamatwa Jumanne iliyopita na kwa kuwa bado yuko kizuizini, hajatoa kauli yoyote.
Polisi walisema Markam alikuwa na uhusiano na mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29 na alikuwa akisisitiza kuwa awe mke wake wa pili.
Lakini familia ya mwanamke huyo ilikataa kupanga ndoa yake mahali pengine.
Polisi wamesema mlipuko huo ulikuwa mkubwa kiasi kwamba kuta na paa la chumba hicho zilianguka kutokana na athari zake.