NA MWANDISHI WETU, DODOMA
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameliomba Bunge liidhinishe bajeti ya sh. 339,361,007,000 ambapo sh. 173,733,110,000 ni kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake na sh. 165,627,897,000 ni kwa ajili ya Mfuko wa Bunge.
Maombi hayo yametolewa leo Aprili 5, 2023 Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Akiwasilisha maombi ya sh. 173,733,110,000 kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake, Waziri Mkuu amesema kati ya fedha hizo, shilingi 121,364,753,320 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 52,368,356,680 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Vilevile ameliomba Bunge liidhinishe sh. 165,627,897,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge ambapo kati ya fedha hizo, shilingi 160,458,877,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 5,169,020,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo
–