NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
SEEIKALI ya Tanzania imekiri kunufaika na Misaada kutoka nchini Marekani kwa miongo sita.
Misaada hiyo kutoka Marekani imesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha ya wananchi katika sekta ya kilimo, elimu, usalama wa chakula, afya, haki za binadamu na utawala bora.
Hayo yameelezwa leo Machi 30, 2023 na Rais Dk Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es salaam.
”Mfano katika sekta ya afya maambukizi ya Ukimwi yamepungua kutoka asilimia 7.2 mwaka 2012 hadi asilimia 4.7 kwa mwaka 2016/17 na yamepungua zaidi mwaka 2021, huku wanawake wajawazito wenye virusi vya ukimwi wanauhakika wa kuzaa watoto wasiokuwa na maambukizi ya ukimwi”amesema na kuongeza
”Katika maralia, vifo vyake vimepungua kutoka Milioni 7.7 kwa mwaka 2015 na kufikia vifo milioni 3.5, tumepunguza nusu ya vifo hivi lengo letu ni kuwa na watu wasiokuwa na maralia kabisa na tupo tayari kupokea mwekezaji yoyote hii kwa sababu tunataka kupunguza mnyororo wa thamani,” amesema.
Amesema Serikali ya Tanzania inapongeza mpango wa Marekani katika kusimamia bahari.”Tunataka wawekezaji katika maeneo mbalimbali ya bahari ikiwemo uvuvi wa bahari,ufugaji,uchimbaji wa chumvi,utalii na usafirishaji,” amesema na kuongeza
”Tunaomba kurejeshwa kwa mkataba wa Agoa ambao unatarajia kumaliza 2025, tunaomba uongezeke muda angalau kwa miaka 10 kwani tukienda hadi 2030 utaweza kutusaidia sana,”amesema