NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inakaribisha utayari wa serikali ya Marekani kufanya mapitio ya mkataba wa Visa wa sasa ili kuwawezesha watanzania kupata visa ya muda mrefu na kufanya biashara,utalii na uwekezaji.
”Suala hili la visa kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa watu na mizigo kati ya nchi zetu mbili Tanzania inakaribisha utayari wa Marekani kufanya mapitio ya mkataba huo ili kuwawezesha raia wa nchi zote mbili kunufaika na visa ya muda mrefu,tuna imani kwamba chini ya mpango huu nchi zetu mbili zitapata mafanikio katika biashara, uwekezaji na utalii” amesema.
Makamu huyo wa Rais amewasili nchini Tanzania Machi 29,2023 majira ya usiku akitokea nchini Ghana na baada ya kukamilisha ziara yake Tanzania anaelekea Zambia ikiwa ni ziara yake ya kwanza barani afrika tangu aliposhika wadhifa huo Januari 2021.