NA JANETH JOVIN, DAR ES SALAAM
MAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema kuwa
amesema uongozi bora hleta utulivu, usalama na utawala wa sheria ambao wawekezaji na wafanyabiashara wengi huzingatia kabla ya kuweka mitaji yao.
Kamala ameyasema hayo leo Machi 30, 2023 Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini jana na leo kupokelewa wa mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan.
Kamala amesema Serikali ya Marekani itakuwa na mkakati mpya wa ushirikiano kiuchumi na Tanzania kutokana na mwenendo mzuri wa masuala ya utawala bora na usimamizi wa haki za binadamu kwani ni vitu ambavyo vinamchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi.