NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
OFISI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imewasilisha kwa Rais hesabu zake leo Jumatano, Machi 29, 2023.
Wakati akiwakilisha hesabu hizo kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022, CAG Charles Kichere amesema katika tathmini ya miaka miwili ya mashirika ya umma ya biashara, mashiriki 14 yalipata hasara.
Kwa mwaka 2020/21, Shirika la Ndege nchini (ATCL) ilipata hasara ya Sh bilioni 36.1 na mwaka 2021/22 Shirika lilipata hasara ya Sh bilioni 35.2.
Shirika la Reli Tanzania (TRC) lilipata hasara ya Sh bilioni 22.8 mwaka 2020/21 na mwaka 2021/22 lilipata hasara ya Sh bilioni 31.2. Kampuni ya Mkulazi ilipata hasara ya Sh.bilioni 5.8 mwaka 2020/21 na mwaka uliofuata ilipata hasara ya Sh bilioni 14.3.
Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) lilipata hasara ya Sh bilioni 26.3 mwaka 2020/21 na mwaka 2021/22 lilipata hasara ya Sh bilioni 11.9.