NAIROBI, KENYA
WATU wasiojulikana wamevamia kampuni ya East Africa Specter Limited katika barabara ya Mombasa jijini Nairobi na kuharibu mali.
Kampuni hiyo ya utengenezaji na kusambaza mitungi ya gesi inasemekana inamilikiwa na familia ya Raila Odinga.
Humphrey Waswa ambaye ni Meneja wa ulinzi na usalama wa kampuni hiyo aliviambia vyombo vya habari kuwa watu zaidi ya 50 walifika kwenye kampuni hiyo wakiwa kwenye pikipiki majira ya saa 11.30 asubuhi na kuwashambulia walinzi waliokuwepo hapo.
“Walikuwa wakisaidiwa na magari manne ambayo hayakuwa na namba za usajili, Land cruiser na tunashuku kuwa lengo lao lilikuwa ni kumdhuru Mkurugenzi wetu mkuu kwa sababu ofisi yake ndiyo imeharibika sana,” amesema Waswa.
Waswa ameongeza kuwa kampuni itatoa taarifa za kina baadaye baada ya uchunguzi kufanyika.
SOMA ZAIDI: