NA BARAKA JUMA, MWANZA
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Geita, Sophiac Jongo amesema halo za manusura wa ajali ya basi la Sheraton iliyotokea Machi 7, 2023 ambao wamelazwa katika Hospitali ya mkoa huo zinaendelea kuimarika inhawa wengine hali sio nzuri.
Kamanda Jongo ameyasema hayo leo Machi 9, 2023 alipozungumza na Demokrasia kwa njia ya simu.
Amesisisltiza kuwa pamoja na hali za majeruhi kuendelea kuimarika hakuna vifo vilivyoongezeka.
Wakati huo huo mwili wa aliyekuwa Mwandish Habari wa Kampuni ya IPP Media Richard Makore ambaye alipoteza maisha katika ajali hiyo unaagwa leo jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari Mkoa wa Mwanza Edwin Sonko , Mwili wa mwandishi huyo utaagwa leo Machi 9, 2023 kwenye Uwanja Pasiansi na kisha kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Serengeti mkoani Mara kwa ajili ya maziko
Makore alipoteza maisha kwenye ajali iliyotokea Machi 07,2023 saa 10 jioni baada ya basi la Sheraton walilokuwa wakisafiria kutoka Mwanza kwenda Ushirombo kupasuka tairi , kuacha njia na kutumbukia darajani eneo la Ibanda Kona, Kata ya Kasamwa mkoani Geita.