NA MWANDISHI WETU, TANGA
CHAMA cha Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) kimemwagia sifa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusema wanauona mkono wa Rais ukiimarisha uhuru wa habari nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu wakati akihutubia kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani la chama chake lililofanyika mkoani Tanga Jumatano Machi 08, 2023.
Ado amesema kila utawala unacho cha kujivunia na kwamba, katika awamu ya sita ya Rais Samia, miongoni mwa kumbukumbu atakazoziacha ni kuitoa tasnia ya habari gizani.
“Unapozungumzia uongozi wa Rais Samia kama mwanamke, tunaweza kuona mifano mingi. Kipindi cha nyuma kidogo tulikuwa gizani; mnajua nyinyi wenyewe hali ilikuwaje?
“Leo unapozungumzia mafanikio ya mchakato wa Mabadiliko ya Sheria ya Huduma za Habari, ndani yake unaona msukumo mkubwa wa Rais Samia. Na katika hili, historia yake ndani ya nchi hii itaandikwa,” amesema Ado.