NA TATU MOHAMED, DAR ES SALAAM
RAIS wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua msanii wa bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mwana FA ambaye ni Mbunge wa Muheza anachukua nafasi ya Pauline Gekul ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Aidha Rais amemteua Ramadhan Kailima kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Kailima anachukua nafasi ya Dk. Wilson Mahera ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 26, 2023 na Katibu Mkuu Kiongozi Dk Moses Kusiluka imesema kuwa Rais Samia amefanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi kwa kuwateua Waziri na Naibu Waziri, Wakuu wa Mikoa, Makatibu na Naibu Makatibu Wakuu pamoja na kumteua Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Wengine walioteuliwa ni Abdallah Ulega ambaye amekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi akichukua nafasi ya Mashimba Ndaki ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Pia Rais amewahamisha Wizara Naibu Mawaziri ambapo Gekul amehamishwa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda kuwa Naibu Waziri Katiba na Sheria. Geofrey Pinda amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na kwenda kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Aidha Ridhiwani Kikwete amehamishwa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenda kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,” amesema
Rais amemuhamisha Deogratius Ndejembi kutoka , Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwenda kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi huku David Silinde akihamishwa kutoka Tamisemi kwenda kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Februari 26, 2023 na Katibu Mkuu Kiongozi, Moses Kusikula imesema kuwa Rais Samia amefanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi kwa kuwateua Waziri na Naibu Waziri, Wakuu wa Mikoa, Makatibu na Naibu Makatibu Wakuu pamoja na kumteua Mkurugenzi wa Uchaguzi.
.
“Viongozi wote walioteuliwa katika nafasi mpya pamoja na Naibu Mawaziri waliohamishwa wizara wataapishwa Februari 27, 2023 saa 10:00 jioni, Ikulu Chamwino,” imehitimisha taarifa hiyo