NA MWANDISHI WETU, DODOMA
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameishauri TCRA kutafuta ufumbuzi wa kudumu ongezeka la utapeli wa mtandaoni.
Akizungumza jijini Dodoma leo, Mei 19, 2023 wakati akiwasilisha bajeti ya wizara kwa mwaka 2023/24 bungeni amesema tatizo la utapeli kwenye mitandao ya simu za mkononi bado ni kubwa nchini.
Sambamba na hayo Waziri Nape ameishauri TCRA kutafuta namna ya kuzuia jumbe fupi zinazotumwa bila idhini au matakwa ya mteja.
Aidha katika hotuba yake Nape aliwasilisha maoni na ushari wa wadau kuhusu uboreshwaji wa Taasisi ambapo miongoni mwa maoni hayo ni kuitaka wizara ishirikiane na makampuni ya mitandao ya simu pamoja na Jeshi la Polisi ili kumaliza tatizo la utapeli wa kimtandao ikiwamo kufungia namba za matapeli pamoja na kushirikiana na vyombo vya dola ili kubaini na kuhakikisha kwamba wahalifu wa makosa ya mitandao wanashitakiwa.
Kwa kuongezea TCRA imeshauri kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi sahihi ya data na vifurushi ili kuondoa malalamiko ya watumiaji wa huduma hiyo