NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti ameipongeza Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa namna ilivyofanya maboresho ya Mitaala ya Elimu nchini yenye lengo la kumfanya muhitimu kuweza kujiajiri au kuajiriwa mara anapomaliza masomo yake.
Magoti ameyasema hayo leo Julai 12,2026 katika maonesho ya Sabasaba ambapo amesema kuwa TET inafanya kazi nzuri ya kuboresha elimu nchini.
“Kwa kweli nawapongeza kwa kazi nzuri ya kuboresha Elimu nchini hasa hivi karibuni katika maboresho ya mitaala yaliyofanyika, ni tumaini langu kwamba wanafunzi nchi nzima wataendelea kufanya vyema, ” amesema Magoti.
Pia ameeleza, anafurahia namna wanafunzi wanaendelea kupatiwa vitendea kazi kama vitabu vinavyowapelekea kuendele kufanya vyema wakati wa masomo yao na kuendelea kuipongeza TET kwa uratibu mzuri na upatikanaji wa vitabu shuleni.
TET inashiriki katika maonesho ya 50 ya Kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba yaliyoanza Juni 28 ambapo yanatarajiwa kufungwa Julai 13.

