Na MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
TANZANIA imeongeza kasi mpya katika mlolongo wake wa usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam, kwenda mikoani na nje ya nchi.
Rais Samia Suluhu Hassan alizindua Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Vigwaza mjini Kibaha takriban kilomita 90 kutoka Dar es Salaam Julai 31, 2025
Sambamba na uzinduzi pia Rais Samia alizindua huduma za usafirishaji wa mizigo kwa Reli ya Standard Gauge (SGR).
Kuunganishwa huko kulifanyika kwa ajili ya kusafirisha sehemu kubwa ya makontena kutoka ukingo wa maji na kuyasogeza sehemu ya nchi kavu kwa njia ya reli kwa ratiba ambayo biashara zinafanyika kwa haraka.
Hatua hiyo imewezesha urahisi wa usafrishaji, ambapo hivi sasa makontena 823 yanasafirishwa kwa siku sawa na makontena 300,000 kwa mwaka.