NA MWANDISHI WETU, DODOMA
MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele amemkabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Wilson Elias Mulumbe.
Mgombea huyo aliambatana na Mgombea Mwenza, Shoka Khamis Juma (kushoto) alichukua fomu hizo Agosti 14, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu.