NA JANETH JOVIN,DAR ES SALAAM
RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania wanapoelekea katika uchaguzi Mkuu kuwa watulivu, kudumisha amani, umoja, mshikamano na kuondoa makundi.
Rais Samia ameyasema hayo leo wakati akizindua hema jipya la Kanisa la Calvary Assemblies of God (Arise and Shine) Kawe jijini Dar es Salaam.
“Tunapoelekea kwenye jambo kubwa lile la demokrasia ya nchi twende tuweke utulivu, amani, Umoja na mshikamano wetu, najua katika jambo lile makundi ni mengi na jana nilikuwa nasoma taarifa ya chama changu wanasema waliochukua fomu za ubunge ni zaidi ya 4000, udiwani karibu 30,000 sasa haya ni makundi mengi
“Tukimaliza shughuli za mchujo wote tunarudi tunakuwa kitu kimoja na tunakwenda kwa pamoja kwenye lile jambo kubwa kwahiyo makundi yale yote ni waumini,” amesema
Rais Samia amesema “Niwaombe sana Maaskofu, wachungaji na viongozi wengine wa dini kusema na waumini kwamba kipindi hichi tutagawana makundi lakini watakaobahatika kuchaguliwa na kupelekwa mbele basi makundi yarudi, Tanzania iwe moja ili tulikabili jambo letu kwa umoja ,” amesema