NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba ameweka wazi kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 utagharamiwa kwa fedha za ndani ikiwa ni ishara ya kujiamini kiuchumi na kuimarika kwa usimamizi wa rasilimali za taifa.
Dk. Mwigulu ameyasema hayo Leo Juni 12,2025 bungeni Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026,.
Waziri wa Mwigulu amesema bajeti hiyo pia inalenga kuendeleza miradi ya kimkakati, kukuza uzalishaji, biashara, na huduma za kijamii kupitia vipaumbele vya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano ambavyo ni kuchochea uchumi shindani na shirikishi.
Amesema bajeti hiyo ina lenga pia kuimarisha uzalishaji wa bidhaa viwandani na utoaji huduma;
kukuza uwekezaji na biashara; na kuchochea maendeleo ya
watu na kuendeleza rasilimali Watu ili kuhakikisha ufikiwaji wa
malengo ya Dira 2025.
Amesema baadhi ya maeneo mahsusi yatakayopewa kipaumbele katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2025/26 ni pamoja na kuendelea kutekeleza na kukamilisha miradi ya kielelezo na
ile ya kimkakati, kuimarisha sekta za uzalishaji zenye matokeo chanya katika kukuza uchumi.
“kuimarisha rasilimali watu hususan katika sekta za huduma za jamii na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini ili kuvutia ushiriki wa sekta binafsi katika shughuli mbalimbali za kiuchumi, maeneo mengine mahsusi ya vipaumbele ni pamoja na ugharamiaji wa Deni la Serikali, mishahara na stahiki za Watumishi wa umma pamoja na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON 2027″
Aidha nipende kuwafahamisha watanzania kuwa Uchaguzi
Mkuu wa Mwaka 2025 tutaugharamia kwa fedha zetu za ndani.