NA MWANDISHI WETU,DODOMA
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Renatus Msangira tuzo ya kutambua mchango wa REA katika kutunza mazingira kupitia utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma,Juni 05,2025.
Miradi hiyo ambayo ni utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ni pamoja na usambazaji wa mitungi ya gesi pamoja na majiko banifu kwa bei ya ruzuku kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa nishati safi ya kupikia vijijini .