NA MWANDISHI WETU, RUVUMA
MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, ( INEC)Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele Mei 03, 2025 ametembelea na kukagua vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali la wapiga kura mkoani Ruvuma katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea na Halmashauri ya Namtumbo ambapo mikoa 15 inaendelea na zoezi hilo.
Mikoa inayoshiriki katika mzunguko wa kwanza wa uboreshaji ni pamoja na Iringa, Geita, Kagera, Mara, Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Rukwa, Tabora, Katavi, Kigoma, Ruvuma, Mbeya, Njombe na Songwe ambapo zoezi hilo limeanza kufanyika kuanzia Mei 1 hadi 7 mwaka huu.