NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Tanzania itaendelea kuwa Mshirika muhimu na wa kimkakati wa nchi ya Italia.
Majaliwa ameyasema hayo leo Juni 09, 2024 alipofanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Tanzania Balozi Marco Lombardi ambaye amemaliza muda wake, Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Balozi Lombardi amesema licha ya kumaliza muda wake kama Balozi wa Italia nchini Tanzania, bado ataendelea kuisemea Tanzania na kuwa mhamasishaji wa fursa zilizopo .