NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula ametoa mhadhara kwa wanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma leo Ijumaa Januari 30 Janua 2026, kwa lengo la kuwaongezea uelewa kuhusu Sheria ya Huduma za Habari.
Katika wasilisho lake, Wakili Kipangula ameeleza majukumu na umuhimu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, akisisitiza wajibu wa wanafunzi na waandishi chipukizi kusoma, kuielewa na kuzingatia Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa wanafunzi kuwa na ithibati na vitambulisho vya uandishi wa habari wakati wote wanapokuwa kwenye mafunzo kwa vitendo (field), ili kuwa na uhalali wa kisheria katika utekelezaji wa majukumu yao ya kihabari.
Akijibu moja ya maswali kuhusu wanafunzi wanaofanya mafunzo katika vyombo vya habari vya vyuo, kama vile Mlimani Radio na Televisheni au SAUT, Wakili Kipangula amesema kuwa, kwa mujibu wa Sheria, wanafunzi hao wanapaswa kuwepo katika vituo hivyo kwa kipindi maalumu cha mafunzo na baada ya kukamilisha mafunzo hayo wanatakiwa kurejea katika ratiba yao ya kawaida ya masomo.







