NA MWANDISHI WETU, SEYCHELLES

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumapili Oktoba 26, 2025 amewasili Seychelles kwa ajili ya kumwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho wa Rais mteule wa sita wa nchi hiyo Dk. Patrick Herminie

Tume ya Uchaguzi ya Taifa ilimtangaza Dk. Patrick Herminie wa Chama cha United Seychelles (US) kuwa mshindi baada ya kumbwaga Rais aliyekuwa madarakani, Wavel Ramkalawan wa Chama cha Linyon Demokratik Seselwa (LDS).

Dk. Patrick Herminie alipata asilimia 52.7 ya kura, huku Rais Wavel Ramkalawan akimaliza wa pili kwa kupata 47.3 ya kura.

