NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary,Péter Szijjártó, leo Jumatatu Septemba 29,2025 wameshuhudia utiwaji saini wa Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) kati ya Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na kampuni ya MeOut Group kutoka Hungary.
Makubaliano hayo, yaliyotiwa saini na Rais wa TCCIA, Vicent Minja, na Mwanzilishi wa MeOut Group,Attila Sandor, yanahusu ushirikiano katika teknolojia ya kilimo na usimamizi wa miradi. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Ushirikiano huu unatarajiwa kuimarisha maendeleo ya sekta ya kilimo kwa kutumia teknolojia za kisasa, pamoja na kuongeza fursa za uwekezaji kati ya Tanzania na Hungary.
Szijjártó yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia baina ya Tanzania na Hungary.