βͺοΈWaziri Mavunde azindua Kiwanda cha kuongeza thamani madini Chumvi Kigoma
βͺοΈNi cha uzalishaji Chumvi Lishe(πΆππ‘π‘ππ πΏπππ) kwa ajili ya Mifugo
βͺοΈLengo ni kupunguza uagizaji wa Chumvi Lishe kutoka nje ya Nchi
βͺοΈTanzania kuongeza uzalishaji wa Chumvi ghafi kwa matumizi ya viwandani
NA MWANDISHI WETU, UVINZA,KIGOMA
WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Nyanza Salt kwa kuitikia wito wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wa uongezaji thamani madini nchini kwa kuanza rasmi uzalishaji wa chumvi lishe itokanayo na madini ya Chumvi mahususi kwa ajili ya kuongeza virutubisho vya mifugo.
Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Agosti 15,2025 wilayani Uvinza mkoani Kigoma wakati akizindua shughuli za Kiwanda cha kuzalisha chumvi lishe(πΎππ©π©π‘π ππππ ) kwa ajili ya mifugo kinachomilikiwa na Kampuni ya Nyanza Salt.
βNi wito wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na matakwa ya sheria juu ya uongezaji thamani madini yetu hapa nchini.
“Nawapongeza Kampuni ya Nyanza kwa hatua hii kubwa ya kuitoa chumvi yetu katika matumizi ya kawaida na kuiongezea thamani kuzalisha Chumvi lishe ambayo ni muhimu kwa virutubisho vya mifugo
“Wafugaji wengi huagiza chumvi lishe kutoka nje ya nchi kwakuwa hakukuwa na uzalishaji hapa nchini,hatua hii ya leo ya uzalishaji wa πΎππ©π©π‘π ππππ nchini itapunguza uagizwaji wa bidhaa hii kutoka nje ya nchi kwa kiwango kikubwa hivyo natoa rai kwa wafugaji kuiunga mkono bidhaa hii inayozalishwa ndani ya ya nchi.
” Tasnia ya chumvi inaendelea kukua kwa kasi siku hadi siku na lengo la serikali ni kuhakikisha tunaboresha mazingira ya uwekezaji kwenye eneo hili ili kuongeza tija na uzalishaji na kuondokana kabisa na uagizaji wa chumvi ghafi kutoka nje ya nchi kama malighafi ya viwandaβ amesema Mavunde
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Nyanza Salt Mines Mukesh Mamlani amesema uzalishaji wa bidhaa ya chumvi lishe itokanayo na madini chumvi ni mkombozi kwa wafugaji wa Tanzania na kwamba kampuni itahakikisha inakidhi viwango na ubora wa bidhaa ili wafugaji wa Tanzania wanufaike.
Pia Mukeshi ameeleza kwamba mpango wa Kampuni ni uzalishaji wa tani 120,000 za chumvi ifikapo mwaka 2027 ili kuhakikisha chumvi ya kutosha inapatikana nchini.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza,Dina Mathamani amesema uwepo wa Kampuni ya Nyanza wilayani Uvinza umekuwa ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi na mapato kwa serikali na wananchi ambapo kupitia Ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja jumla ya wa wananchi 1000 wamekuwa wakipata Ajira kiwandani hapo wakati wa msimu wa uchakataji chumvi.