NA MWANDISHI WETU,DODOMA
MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ( INEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele amekabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo.
Mgombea huyo wa NLD aliambatana na Mgombea Mwenza, Chausiku Khatib Mohamed kuchukua fomu hizo leo Jumapili Agosti 10,2025 ambapo Tume inatarajia kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu
Katika hatua nyingine,Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mwambegele amemkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Makini (MAKINI), Coster Jimmy Kibonde.
Mgombea huyo wa MAKINI aliambatana na Mgombea Mwenza, Aziza Haji Suleiman
Tukio hilo lilishuhudiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ramadhan Kailima.