NA MWANDISHI WETU,DODOMA
MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele amemkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP),Kunje Ngombale Mwiru.
Mgombea huyo wa AAFP aliambatana na Mgombea Mwenza, Shum Juma Abdalla amechukua fomu hizo leo Jumamosi Agosti 9,2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu.