NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Latifa Khamis ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Biashara na Uchumi.
Dk. Latifa ametunukiwa shahada hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika kukuza biashara na diplomasia ya uchumi kati ya Tanzania na nchi nyingine.
Tuzo hiyo imetolewa na London Institute of Skills Development and Oxford Club kama uthibitisho wa juhudi, umahiri na mafanikio ya Dk. Latifa katika kusimamia kwa ufanisi majukumu ya TanTrade, ambayo yamechochea maendeleo ya sekta ya biashara nchini na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa wa kiuchumi.