NA MWANDISHI MAALUM, DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto Biteko, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk. Moses Kusiluka kwenye picha ya pamoja na Mawaziri mara baada ya Kikao cha mwisho cha Baraza la Mawaziri cha Serikali ya Awamu ya Sita kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma Leo Julai 14 , 2025.