NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa viwanda na biashara, Dk.Selemani Jafo(MB) ametembelea banda la Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo Tanzania(TCCIA)katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) yanayoendelea jijini Dar es salaam jana.
Dk.Jafo alijionea na kupata ufafanuzi wa shughuli,huduma na elimu vinavyotolewa na TCCIA kutoka kwa Meneja wa Viwanda Ezekiel Kahatana pamoja na wafanyakazi wa Taasisi hiyo.
Pia Dk.Jafo alisaini kitabu cha wageni wanaofika na kutembelea banda la TCCIA.