NA MWANDISHI WETU,KIGOMA
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 13, 2025 ametembelea kituo cha kulea watoto wenye uhitaji cha Sanganigwa kilichopo mjini Kigoma, kinachosimamiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma.
Akizungumza na watoto na walezi wa kituo hicho, Majaliwa amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan inatambua mchango wa madhehebu ya dini katika kuwalea kimwili na kiroho watoto wenye mahitaji maalum nchini.
“Kwa niaba ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ninalishukuru kanisa katoliki jimbo la Kigoma, mtu mmoja mmoja na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa Serikali katika kuwalea watoto wetu, hakika mnafanya jambo kubwa na la kumpenda Mungu na wanadamu”
Akisoma taarifa ya kituo hicho kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi wa Kituo hicho Keneth Hageze amesema kuwa kilianzishwa mwaka 1995 na hadi sasa kimehudumia watoto 1309.
Majaliwa alitoa Mchele, Maharagwe, Mafuta, Sukari pamoja na Taulo za kike.